Quantcast
Channel: Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3230

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

$
0
0


220px-Coat of arms of Tanzania.svg f1f71


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MKUTANO WA MAWAZIRI WA BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA AFRIKA

1.             Mkutano wa Mawaziri wa  Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) utafanyika hapa Dar Es Salaam tarehe 22 Aprili, 2013. Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2.             Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika lina wajumbe 15 kutoka kwenye Kanda zote tano za Umoja wa Afrika. Wajumbe hao ni Algeria, Angola, Cameroon, Congo (Barazzaville), Cote d’Ivoire, Djibouti, Equatorial Guinea, Gambia, Guinea, Lesotho, Misri, Msumbiji, Nigeria Uganda na Tanzania.

3.             Baraza hilo litakalokutana  chini ya Uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamillius Membe, litajadili pamoja na mambo mengine, hali ya kisiasa nchini Madagascar ambayo iliathiriwa vibaya na mapinduzi yaliyofanyika nchini humo mwezi Machi, 2009.

4.             Mkutano huo muhimu unatarajiwa kupendekeza mikakati ya kusaidia Madagascar kufanya uchaguzi huru na wa haki mwezi Julai, 2013.



IMETOLEWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA 

KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.

20 APRILI 2013







Viewing all articles
Browse latest Browse all 3230

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>