Mhe. Dkt. Damas Ndubaro (Mb) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo amekabidhiwa rasmi Wizara hiyo na aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Suzan A. Kolimba (Mb), hafla ya makabidhiano ilifanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtaa wa Makole jingo la LAPF jijini Dodoma. Katika hafla ya makabidhiano walihudhuria Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo waliosimama nyuma ya viongozi hao. |