Quantcast
Channel: Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3230

Waziri Membe amuenzi Marehemu Brigedia Generali Hashim Mbita

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Bregedia Generali Hashim Mbita, kilichotokea hivi karibuni katika Hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam. Marehemu Brigedia Generali Mbita aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambabwe pia atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwenye harakati za ukombozi Barani Afrika.
Waziri Membe akimpa pole Mjane wa Marehemu Bregedia Generali Mbita, Bi. Ngeme Mbita  
Mhe. Membe akimpa pole mtoto wa Marehemu Brigedia Generali Mbita Bi. Sheilla Mbitta
Waziri Membe akizungumza na wafiwa 
Waziri Membe akisalimiana na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini mara baada ya kuwasili kwenye  Msiba wa Brigedia Generali Hashim Mbita
Waziri Membe akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zuberi Zitto Kabwe walipokutana kwenye msiba wa Brigenida Generali Mbita 
Waziri Membe akiwa amejumuika  na Waombolezaji wengine kwenye msiba wa Brigedia Generali Mbitta nyumbani kwake Chang'ombe Jijini Dar es Salaam
Waziri Membe akizungumza na waandishi wa Habari juu ya kifo cha Brigedia Generali Mbita. Waziri Membe alimwelezea Balozi Mbita kama kiongozi makini na mwadilifu na pia alikuwa mwanaharakati mahiri ambaye alihakikisha Bara lote la Afrika linakuwa huru.



Picha na Reginald Philip


Viewing all articles
Browse latest Browse all 3230

Trending Articles