Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Msumbiji nchini, Mhe. Vicente Veloso alipofika Wizarani kwa ajili ya kuzungumza na Balozi Mulamula kuhusu namna bora ya kuiamarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Msumbiji na pia kumpongeza kwa kuteuliwa na Rais kuwa Katibu Mkuu.
Mkutano ukiendelea huku wajumbe kutoka pande zote mbili wakisikiliza kwa makini. Wa pili kulia ni Bi. Zuhura Bundala, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bi. Talha Mohammed (kulia), Afisa Mambo ya Nje.