Quantcast
Channel: Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation
Viewing all 3230 articles
Browse latest View live

Tanzania Yashiriki Maadhimisho ya Miaka 25 ya IORA

$
0
0

Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika  Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amewasilisha kwa njia ya mtandao salamu za pongezi ya Miaka 25 ya Jumuiya ya Nchi Wanachama wa Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Assocaition-IORA) yaliyofanyika jijini Mapou, Mauritius tarehe 7 Machi 2022.

Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki imewakilishwa na Balozi Agnes Richard Kayola, Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda aliyeambatana na Dkt. Mnata Resani,  Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Katika Maadhimisho hayo, nchi wanachama zimepata fursa ya kutangaza Utamaduni wao kwa kupitia vyakula, nyimbo na ngoma za asili. Tanzania iliandaa chai na kahawa ya hapa nchini na Kikundi cha ngoma kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) kilitumbwiza kwenye maadhimisho hayo.


Watu mbalimbali wakichukua vyakula vya Kitanzania vilivyoandaliwa kwa ajili ya kuadhimisha miaka 25 ya Jumuiya ya Nchi Wanachama wa Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Assocaition-IORA) yaliyofanyika jijini Mapou, Mauritius tarehe 7 Machi 2022.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Mhe. Alan Ganoo
 akitoa neno wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 25 ya umuiya ya Nchi Wanachama wa Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Assocaition-IORA) yaliyofanyika jijini Mapou, Mauritius tarehe 7 Machi 2022.

Mkurugenzi wa Idara ya Ushrikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Agnes Kayola akiwa na wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Mauritius.


UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ITALIA WAKUTANA NA WANADIASPORA

$
0
0

 Na Mwandishi wetu, Roma

Ubalozi wa Tanzania nchini Italia umekutana na kufanya Mkutano Mkuu na Jumuiya mbalimbali za Watanzania wanaoishi maeneo mbalimbali nchini Italia (Diaspora) kwaajili ya kuimarisha mahusiano na ushirikiano baina ya pande mbili.

Akifungua mkutano huo mwishoni mwa wiki, Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo alitoa wito kwa Watanzania hao kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuiletea Tanzania maendeleo.

“Nawashauri kujisajili katika daftari la Diaspora wa Italia ili kuwa na takwimu na kumbukumbu sahihi za Watanzania waliopo Italia. Takwimu na kumbukumbu hizi zitasaidia Ubalozi kuwaunganisha Wanadiaspora na wabia wa maendeleo ambao wana nia au tayari wanaendesha shughuli zao nchini Tanzania na wanahitaji kushirikiana na Diaspora,” Amesema Balozi Kombo.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo ulijadili masuala mbalimbali yanayowahusu wanadiaspora ikiwemo changamoto za kiutendaji na ushirikiano katika Jumuiya zao ambazo zilianishwa wazi kwenye taarifa za kiutendaji zilizowasilishwa na Viongozi wa Jumuiya.

Mkutano uliazimia kuendelea kuimarisha mahusiano na ushirikiano baina ya Wanadiaspora na Ubalozi kwa kuanisha mkakati thabiti wa kuboresha mawasiliano baina ya pande mbili.

Aidha, wanadiaspora hao wameahidi kuendelea kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Italia  katika kuiletea nchi yao maendeleo kwa kuwekeza nchini kwao. Kadhalika, Ubalozi umeahidi kutafuta suluhu ya kudumu dhidi ya changamoto zinazowakabili wanadiaspora waishio nchini Italia.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na wanadiaspora takriban 100 akiwemo Mhashamu Baba Askofu Mkuu Protase Rugambwa, Katibu Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu.

Nchini Italia zipo Jumuiya sita zinazotoka maeneo ya Roma, Napoli, Modena Central North, Genova, Modena na Umoja wa Watanzania Wakatoliki unaojumuisha Waklero, Watawa, Waseminari na walelewa wa Utawa wanaofanya kazi za kitume hapa Italia.

Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiongea na Wanadiaspora (hawapo pichani) wanaoishi nchini Italia wakati wa Mkutano 

Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma akiwasilisha Bi. Anastacia Lubangila, taarifa ya Jumuiya hiyo wakati wa mkutano


Mhashamu Baba Askofu Mkuu, Protase Rugambwa akifuatalia majadiliano


Mwenyekiti Kamati Kuu ya Wanadiaspora Italia Bw. Maulid Kagutta, akiwasilisha taarifa ya Diaspora Italia 


Balozi Kombo akipokea picha ya nembo rasmi ya Jumuiya ya Watanzania Genova kutoka kwa Bi. Eva Nangela, Mwenyekiti wa Jumuiya (kushoto). Wanaoshuhudia (kulia) ni Bi. Zakia Kombo, Mwenza wa Mhe. Balozi; Baba Askofu Mkuu Rugambwa na Maafisa Ubalozi, Bw. Sigfried Nnembuka pamoja na Jacqueline Mbuya. 


Wanadiaspora wakifuatilia mkutano

Wanadiaspora wakifuatilia mkutano



TAARIFA KUHUSU WANAFUNZI RAIA WA TANZANIA WALIOKWAMA NCHINI UKRAINE

WAZIRI MULAMULAZIARANI NCHINI SAUDI ARABIA

$
0
0

 

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kushoto) akimsikiliza Bw. Hussyan Alrashid , Mkurugenzi wa Idara ya Afrika - Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia (katikati) katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa jjini Riyadh alipompokea Mhe. Waziri Mulamula alipowasili nchini Saudi Arabia

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa na mwenyeji wake kulia akizungumza alipowasili katika uwanja wa ndege wa jijini Riyadh nchini Saudi Arabia kuanza ziara ya kikazi nchini humo, wa kushoto kwa Mhe. Waziri ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki na wa kwanza kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa na mwenyeji wake kulia akizungumza alipowasili katika uwanja wa ndege wa jijini Riyadh nchini Saudi Arabia kuanza ziara ya kikazi nchini humo, wa kushoto kwa Mhe. Waziri ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki na wa kwanza kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) katika kikao cha paamoja na timu aliyoambatana  nayo nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kujipanga kwa pamoja wakati wa ziara ya kikazi nchini humo mara baada ya kuwasili.  Kushoto  ni Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini  akimsikiliza.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (wa kwanza kulia) Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi  Hemedi Mgaza (wa pili kutoka kulia) akiwa na maafisa wengine wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia hayupo pichani wakati wa kikao cha pamoja kuhusu ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania nchini Saudi Arabia mara baada ya kuwasili nchini humo

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini  (katikati) akizungumza katika kikao cha kujipanga huku Waizri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (kushoto ) akimsikiliza na kulia kwa Mhe. Balozi ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda nchini (TCCIA )Bw. Pal Koyi  akiandika yanayojiri.


 

 

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, amewasili nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 9 hadi 12 Machi 2022. Ziara hiyo inafuatia mualiko uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud, alipotembelea Tanzania mwezi Machi 2021. 

Katika ziara hiyo Balozi Mulamula ameambatana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na wawakilishi wa wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima kutoka Tanzania Bara.

Akiwa nchini Saudi Arabia Mhe. Waziri Mulamula anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud na Waziri wa Biashara na Uwekezaji Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi,  viongozi wengine wanaosimamia sekta za sekta za Mifugo na Utalii na wafanyabiashara  na wenye viwanda wa Saudi Arabia.

Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia pia kukutana na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini humo na wafanyabiashara marafiki wa Tanzania mjini Riyadh.

Balozi Mulamula na ujumbe wake pia wanatarajia kukutana na kuzungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa miji ya Jeddah na Makkah katika mkutano utakaofanyika jijini Jeddah..

Balozi Mulamula na ujumbe wake watarejea nyumbani tarehe 13 Machi 2022.

 

 

 

 

VACANCY ANNOUNCEMENT

WAZIRI MULAMULA AKUTANA NA WAZIRI WA BIASHARA NA UWEKEZAJI WA SAUDI ARABIA

$
0
0

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza katika kikao na Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi na ujumbe wake hawapo pichani walipokutana katika ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (wa pili kulia ) akizungumza katika kikao na Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia (hawapo pichani) wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Hemedi Mgaza. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini akifuatilia mazungumzo hayo katika kikao kilichofanyika jijini Riyadh
Ujumbe wa Saudi Arabia (kushoto) katika kikao cha pamoja na ujumbe wa Tanzania (kushoto) walipokutana katika Ofisi za Wizara ya Biashara na Uwekezaji jijini Riyadh

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (wa nne kutoka kushoto) akizungumza katika kikao na Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi na ujumbe wake hawapo pichani walipokutana katika kikao jijini Riyadh.

 

Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi (wa pili kushoto) akiwa  na ujumbe wake akizungumza katika kikao na Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake hawako pichani walipomtembelea ofisini kwake jijini Riyadh

 



Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi akimpa zawadi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula baada ya  kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh- Saudi Arabia.

Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabiakimpa zawadi Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh- Saudi Arabia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, akimpa zawadi Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi baada ya  kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh- Saudi Arabia.

Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi  Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi (aliyenyoosha mikono) akielezea jambo wakati akiwasindikiza Waziri Mulamula na ujumbe wake mara baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo jijini Riyadh nchini humo.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Biashara na Uwekezaji Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh- Saudi Arabia.

Waziri Mulamula amemuhakikishia Mhe. Dkt. Al-Qasabi utayari wa Tanzania katika kushirikiana na Saudi Arabia kuptia sekta za mifugo, uvuvi, uwekezaji na usafiri wa anga.

Katika ziara hiyo Balozi Mulamula ameambatana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Mkurugenzi wa Idara ya Mashriki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Hemedi Mgaza, kaimu Mkurugenzi Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)  Bibi Anna Lyimo na wawakilishi wa wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima kutoka Tanzania Bara .

Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia pia kukutana na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini humo na wafanyabiashara marafiki wa Tanzania walioko jijini Riyadh.

Balozi Mulamula na ujumbe wake pia wanatarajia kukutana na kuzungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara walioko katika miji ya Jeddah na Makkah katika mkutano utakaofanyika jijini Jeddah.

Waziri Mulamula na ujumbe wake waliwasili nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi tarehe 9 ikiwa ni mualiko uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud, alipotembelea Tanzania mwezi Machi 2021.  Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia kurejea nyumbani tarehe 13 Machi 2022.

 

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA MWANA MFALME WA SAUDI ARABIA

$
0
0

 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kushoto) aliyekwenda Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia jijini Riyadh kuonana naye wakati wa ziara ya kikazi nchini humo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud (kulia) alipowasilli katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia jijini Riyadh.             
 

 

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula ukiwa nje ya Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia baada ya kumalizika kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud ulipokwenda kuonana naye katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia jijini Riyadh

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika picha na makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi Arabia Bw. Tariq Al Haidary walipokutana jijini Riyadh

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja kabla ya kikao na viongozi wa Shirikisho la wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi Arabia kilichofanyika katika Ofisi za Shirikisho hlo jijini Riyadh.

 

Balozi Liberata Mulamula akizungumza katika  kikao na viongozi wa Shirikisho la wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi Arabia kilichofanyika katika Ofisi za Shirikisho hilo jijini Riyadh

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Hemedi Mgaza (katikati) na Afisa Dawati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Davis Byarugaba wakifuatilia kikao na Shirikisho la  Wafanyabiashara na wenye viwanda Saudi Arabia
Ujumbe wa Tanzania ukikabidhi zawadi kwa Makamu mwenyekiti wa Shirikisho la  wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi Arabia Bw. Tariq Al Haidary baada ya kikao na viongozi wa shirikisho hilo kilichofanyika katika Ofisi za Shirikisho hilo jijini Riyadh

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akipokea zawadi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi Arabia Bw. Tariq Al Haidary baada ya kikao na viongozi wa shirikisho hilo kilichofanyika katika Ofisi za Shirikisho hlo jijini Riyadh

Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa Shirikisho la wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi Arabia baada ya kikao na viongozi wa shirikisho hilo kilichofanyika katika Ofisi za Shirikisho hilo jijini Riyadh

 

Na mwandishi wetu, Riyadh

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud alipomtembelea katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh- Saudi Arabia.

Katika mazungumzo yao Waziri Mulamula amemuhakikishia mwenyeji wake Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud kwamba Tanzania iko tayari kushirikiana na Saudi Arabia na kuendelea kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo.

Balozi Mulamula pia amemuhakikishia mwenyeji wake juu ya utayari wa Tanzania katika kufanya biashara na Saudi Arabia ikiwa ni pamoja na kuelezea fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania kupitia sekta za mifugo, uvuvi, kilimo, utalii na usafiri wa anga.

Naye Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud alimuhakikishia Mhe Waziri juu ya nia na utayari wa Saudi Arabia kufanyabiashara na kuwekeza Tanzania kwa ajili ya kuzinufaisha nchi zote mbili.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa Tanzania na Saudi Arabia kuendelea kushirikiana na kuhakikisha biashara za uwekezaji vinashamiri baina ya nchi hizo.

Katika hatua nyingine Waziri Mulamula amekutana na viongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara na wenye viwanda wa Saudi Arabia jijini Riyadh na kuelezea fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana nchini na kuainisha maeneo ya kipaumbele kwa sasa.

Maeneo yaliyoainishwa kama kipaumbele katika kikao hicho ni pamoja na kilimo, mifugo, uvuvi, utalii na usafiri wa anga.

Waziri Muamula ametumia kikao hicho kuwaalika nchini wanachama wa jumuiya hiyo kwa ajili ya kushiriki Maonesho ya Kimaatafa ya Biashara ya Dar es Salaam maarufu Sabasaba yanayofanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam mwezi Julai

Viongozi wa jumuiya hiyo wameshukuru kupata nafasi ya kuonana na ugeni huo kutoka Tanzania ambao ulijumuisha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara na wenye viwanda nchini (TCCIA) Mr. Joseph Koyi, kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) bibi Anna Lyimo na wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka Tanzania Bara.

 Waziri Mulamula na Ujumbe wake wako nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud, alioutoa mwezi Machi 2021 alipotembelea Tanzania. 

Katika ziara hiyo Balozi Mulamula ameambatana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro,  mwakilishi wa TAWA, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na wawakilishi wa Wafanyabiashara na Wenye Viwanda nchini.

Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia pia kukutana na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia, wafanyabiashara marafiki wa Tanzania wa jijini Riyadh na Jumuiya ya Wafanyabiashara katika miji ya Jeddah na Makkah atakaokutaana nao jijini Jeddah. Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia kurejea nyumbani tarehe 13 Machi 2022.

 

 

 

 

 

 

 


 


 

 

 

 

 

 

 


WAZIRI MULAMULA ATEMBELEA OFISI ZA UBALOZI WA TANZANIA SAUDI ARABIA

$
0
0
Waziri wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula alipowasili katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia jijini Riyadh na kuzungumza na watumishi wa Ubalozi huo.
Balozi Liberata Mulamula (katikati) akiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini  (kulia) wakiangalia picha ukutani (hazipo ktika picha) walipowasili katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Riyadh kwa ajili ya kukagua ubalozi huo na kuzungumza na watumishi.
Balozi Liberata Mulamula (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini  (wa kwanza kulia) huku Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Hemedi Mgaza (kushoto) akifuatilia mazungumzo hayo.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini  (kulia) akiwaonesha kitu Balozi Liberata Mulamula (katikati) na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kushoto) walipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Riyadh .
Balozi Liberata Mulamula akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Riyadh alipotembelea na kuzungumza na watumishi wa Ubalozi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia walipotembelea Ofisi hizi jijini Riyadh .
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia alipotembelea Ofisi hizo jijini Riyadh.
kikao kikiendelea katika Ofisi za Ubalozi jijini Riyadh

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (katikati) katika picha ya pamoja na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia alipotembelea Ofisi hizo jijini Riyadh.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (katikati) katika picha ya pamoja na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia alipotembelea Ofisi hizo jijini Riyadh.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ametembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia nchini humo.

Akizungumza na Watumishi wa Ubalozi jijini Riyadh, Balozi Mulamula amewataka kuzingatia ulinzi wa taswira ya nchi yao hasa kwa kuzingatia mienendo ya maisha yao na kauli zao pia.

“Chochote mnachofanya ndio sura na kioo cha Jamhui ya Muungano wa Tanzania huku, nawaombeni sana kuzingatia hilo, japo ni kweli kwa mienendo yenu hatuwaingilii lakini hamna budi kujua kuwa nyie ni taswira ya nchi yetu huku,” alisema Balozi Mulamula.

Balozi Mulamula pia amewataka watumishi hao kuhakikisha wanafuata na kuzingatia misingi na kanuni za utumishi wa umma licha ya kutekeleza majukumu yao nje ya Tanzania.

Pia amewataka Mabalozi na watumishi walioko katika balozi za Tanzania kuendela kuwa walezi wa Watanzania popote walipo na kuwa tayari kuwasaidia pale watakapohitaji msaada kutoka katika balozi hizo.

Waziri Mulamula yuko nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud, alioutoa mwezi Machi 2021 alipotembelea Tanzania na anataarajia kurejea nyumbani tarehe 13 Machi 2022.  
 
Katika ziara hiyo Waziri Mulamula ameambatana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki , kituo cha Uwekezaji nchini na Chama cha cha wafanyabiashara na wenye viwanda nchini (TCCIA)










  

 


WAZIRI MULAMULA AKUTANA NA WATANZANIA WANAOISHI SAUDI ARABIA

$
0
0

 

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini (kushoto) akiwa amekaa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Nyumbani kwake jijini Riyadh wakati alipomualika Mhe. Waziri kuzungumza na Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia wakati Waziri Mulamula alipokuwa na ziara ya kikazi nchini humo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na viongozi wa Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia wakati alipokutana nao nyumbani kwa Mhe. Balozi Mwadini jijini Riyadh
Mwakilishi wa Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia Bi Amina akisoma risala kwa Balozi Mulamula wakati alipokutana na Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia  nyumbani kwa Balozi wa Tanzania jijini Riyadh 
Bi Amina akiwasilisha nakala ya risala aliyoisoma kwa Mhe. Waziri Mulamula alipokutana na Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia nyumbani kwa Balozi wa Tanzania jijini Riyadh

Mwakilishi wa Watanzania wanawake wanaoishi nchini Saudi Arabia akimkabidhi zawadi Balozi Mulamula wakati alipokutana na Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia  nyumbani kwa Balozi wa Tanzania jijini Riyadh 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia Dkt. Msechu akimkabidhi zawadi Balozi Mulamula wakati alipokutana na Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia  nyumbani kwa Balozi wa Tanzania jijini Riyadh  

 

Balozi Mulamula mwenye (ushungi wa bluu) akiwa na Waziri wa Maliasili na Utaalii Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (kushoto) Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kulia) pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia wakati walipokutana na Mawaziri hao nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini jijini Riyadh.

 


 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia na kuwataka kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa Tanzania nchini humo.

Balozi Mulamula amekutana na Watanzania hao jijini Riyadh katika kikao kilichofanyika nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini.

Akizungumza na Watanzania hao Balozi Mulamula amesisitiza juu ya umuhimu wa Watanzania hao kuishi kwa kufuata sheria na kanuni za nchi hiyo kwani kufanya hivyo kutaendelea kulinda taswira nzuri ya nchi yao.

Balozi Mulamula pia amewahahakishia watanzania hao juu ya nia ya Serikali ya kufanyia kazi mawazo na maoni yao ili kuwa kuwa na amani.

‘’Niwahakikishieni ndugu zetu mlioko huku, serikali yenu ni sikivu inathamini na kujali maoni mnayoyatoa na inayafanyia kazi, na muda si mrefu mtaona tulipofikia,” alisema Balozi Mulamula.

Awali katika risala yao kwa mhe. Waziri Watanzania hao walielezea changamoto na mafanikio yaliyopatikana kupitia umoja wao na kuiomba serikali kufanyia kazi changamoto wanazozipata hasa wakati wa kuondoka nyumbani.

Waziri Mulamula yuko nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud, alioutoa mwezi Machi 2021 alipotembelea Tanzania.

 

 

BALOZI SOKOINE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU WA SADC MJINI LILONGWE, MALAWI

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph E. Sokoine akiongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha kawaida cha Baraza la Mawaziri wa SADC kinachofanyika Lilongwe nchini Malawi. Nyuma ya Balozi Sokoine kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Exavier Daudi anayefuata ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agnes Kayola pamoja na Afisa dawati.



Kikao cha Makatibu Wakuu kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kikiendelea katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Bingu wa Mutharika Lilongwe, Malawi

 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa uwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha Makatibu Wakuu wa SADC. Kushoto kwa Balozi Sokoine ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Bw. Exavier Daudi na kulia kwa Balozi Sokoine ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Shaaban
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine ukijadili mwenendo wa kikao cha Makatibu Wakuu wa SADC kuhusu maslahi ya Tanzania, Lilongwe, Malawi

BALOZI WA MAREKANI APONGEZA UENDESHAJI MICHAKATO YA KISIASA NCHINI

$
0
0

 

Na Waandishi wetu, Dar


Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Donald Wright amepongeza uendeshaji wa michakato ya kisiasa inavyoendeshwa nchini Tanzania. 

Balozi Wright ameyasema hayo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Wright amesema anaridhishwa na jinsi hali ya kisiasa ilivyo hapa nchini na kuongeza kuwa anaunga mkono michakato ya kisiasa inavyoendeshwa nchini na kuelezea kuridhishwa kwake na hali hiyo. 
 
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani kwa maslahi ya pande zote mbili. 

Naye Waziri Mulamula amemuahidi Dkt. Wright kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake wakati wote hapa nchini.

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Mhe. Elisabeth Jacobsen na kujadili masuala ya ushirikiano katika masuala ya amani na usalama, jinsia na uwezeshaji wa wanawake.

Pia, Waziri Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Afisa kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bibi. Jacqueline Machangu-Motcho na kujadili masuala ya ushirikiano baina ya mfuko huo na Tanzania.

Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Donald Wright akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Donald Wright  

Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Donald Wright kikiendelea

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Norway nchini Mhe. Elisabeth Jacobsen katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza Afisa kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bibi. Jacqueline Machangu-Motcho katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



BALOZI MULAMULA ATAJA MAFANIKIO WIZARA YA MAMBO YA NJE

$
0
0

Na Waandishi Wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ametaja maeneo 11 ambayo Wizara inajivunia katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita madarakani chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. 

Akiongea na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Balozi Mulamula amesema Wizara ya Mambo ya Nje katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Wizara imetekeleza majukumu yake kwa mafanikio.

Balozi Mulamula ameyataja mafanikio hayo kuwa ni kusainiwa kwa makubaliano na mikataba ya ushirikiano katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa kufuatia ziara mbalimbali zilizofanywa na viongozi wa Kitaifa nje ya nchi na Wakuu wa nchi na Mashirika ya Kimataifa kutembelea nchini. 

“Ziara hizo pia zimewezesha upatikanaji wa misaada na mikopo ya masharti nafuu ambapo fedha kiasi cha Shilingi Trilioni 1.77 na Euro milioni 425 kutoka Kamisheni ya Umoja wa Ulaya zilipatikana, wakati huohuo Tanzania ilichaguliwa na nchi 192 wanachama wa Umoja wa Mataifa kuwa Makamu wa Rais wa Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambapo katika uchaguzi huo, Tanzania ilipita bila kupingwa, mara ya mwisho Tanzania kupata nafasi hiyo ilikuwa mwaka 1991,” amesema Balozi Mulamula.

Mafanikio mengine ni kufunguliwa kwa Balozi mpya mbili katika nchi za Austria na Indonesia na Konseli Kuu tatu katika miji ya Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Shanghai na Guangzhou nchini China, ikiwa ni pamoja na ukarabati wa majengo katika balozi za Tanzania.

Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa wawekezaji kutoka nje ambapo wengi wameonesha dhamira ya kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali. 

Balozi Mulamula amesema Lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza kiswahili kimetambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kuwekewa siku maalum ya kuadhimishwa duniani ambayo ni tarehe 7 Julai kila mwaka. Niwakumbushe kuwa, Kiswahili ni lugha ya kwanza ya kiafrika kupewa hadhi hiyo na UNESCO," Amesisitiza Balozi Mulamula.

Mafaniko mengine yaliyoainishwa na Mhe. Waziri wakati wa mkutano huo ni pamoja na kuondolewa kwa vikwazo 56 kati ya 64 vya kibiashara kufuatia maagizo ya Marais wa Kenya na Tanzania. Aidha, vikwazo vingine vinane viliondolewa na Mawaziri wa Biashara wa nchi hizi mbili walipokutana Zanzibar tarehe 13 Machi 2022.

Kadhalika, Waziri Mulamula amesema Wizara yake itaendelea kutekeleza Sera ya Mambo ya Nje hususan kwenye masuala ya kukuza uchumi wa nchi kwa kuhamasisha uwekezaji kutoka nje, biashara na utalii. 

Balozi Mulamula amehitimisha na Suala la Watanzania waliokuwa wamekwama nchini Ukraine ambapo amesema serikali imechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha raia wake wanakuwa salama pamoja na changamoto hizo. 

“Napenda kuwafahamisha kuwa, zoezi la kuwaondoa Watanzania wote waliokuwepo nchini humo wakiwemo Wanafunzi limekamilika ambapo hadi sasa takribani Watanzania 300 wamefanikiwa kuondoka na kuelekea nchi jirani na baadhi yao wamerejea hapa nchini”, amesema Balozi Mulamula.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akisikiliza moja kati ya maswali yaliyoulizwa na baadhi ya waandishi wa habari (hawapo pichani) alipowasilisha taarifa ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita  


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiongea na waandishi wa habari  alipokuwa akiwasilisha taarifa ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita  




KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA KUSAIDIA KUWAREJESHA WANAFUNZI WALIOKUWA NCHINI UKRAINE

$
0
0
Na Waandishi Wetu, Dar 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) imeipongeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa juhudi ilizozichukua hadi kufanikisha zoezi la kuwarejesha salama wanafunzi waliokuwa nchini Ukraine.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Vita Kawawa (Mb) Jijini Dar es Salaam wakati Kamati hiyo ilipotembelea Chuo cha Diplomasia (CFR).

Katika Kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula pamoja na Naibu Katibu Mkuu Mhe. Balozi Fatma Rajab.
“Nichukue nafasi hii kutoa pongezi nyingi kwa Wizara kwa jinsi mlivyoshughulikia suala zima la kuhakikisha wanafunzi wa Kitanzania walioko nchini Ukraine wanarejea salama nchini,” amesema Mhe. Kawawa.

‘’Mhe. Waziri tunawapa pongezi nyingi, kwa kazi  na hatua kubwa mlizochukua  na jinsi mlivyoshirikiana na wazazi wenye wanafunzi waliokuwa wanasom nchini Ukraine hasa ikizingatiwa kuwa wazazi hao waliwapeleka watoto wao binafsi bila ya kuishirikisha Serikali,’’ ameongeza Mhe. Kawawa.

Amesema kamati imeridhishwa na jinsi ambavyo Wizara ilivyosimama imara na kuwasaidia Watanzania wote waliokuwepo nchini Ukraine na kuhakikisha wanarejea nyumbani salama.

Mhe. Kawawa ametoa wito kwa Watanzania wanapokuwa nje ya nchi kujiandikisha katika Balozi za Tanzania ili kuwa rahisi kuwaratibu pale inapotokea athari yoyote kule wanapokuwepo.

Mhe. Kawawa amewapongeza vongozi wa wizara, mabalozi na watumishi wa wizara ambao kwa namna moja au nyingine wamefanikisha uondoaji wa watanzania waliokuwepo nchini Ukraine.
Akizungumza katika kikao hicho Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameihakikishia kamati hiyo kwamba Uongozi wake utaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha inasimamiwa ili ikamilike kwa wakati na kuendana na thamani halisi ya fedha iliyotolewa na Serikali.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa katika Chuo cha Diplomasia (CFR) Jijini Dar es Salaam

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula wakikagua mradi wa ujenzi wa vyumba vya mihadhara ya Chuo cha Diplomasia (CFR) Jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea Chuo Cha Diplomasia Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula. 

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Alexander Mnyeti akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea Chuo Cha Diplomasia Jijini Dar es Salaam

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Stella Ikupa akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea Chuo Cha Diplomasia Jijini Dar es Salaam

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU)  katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula, Naibu Katibu Mkuu Balozi Fatma Rajab pamoja na viongozi wa Chuo  Cha Diplomasia Jijini Dar es Salaam





 

WAZIRI MULAMULA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA BALOZI WA MALAWI

$
0
0

Na Waandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amepokea nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Baada ya kupokea nakala ya hati hizo Balozi Mulamula amemuahidi Balozi mteule ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake ya kibalozi wakati wote atakaokuwepo nchini.

“Leo nimepokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Malawi na tumefarijika kwa Mhe. Rais Chakwera kumteua Balozi huyu mara baada ya Balozi wa awali kumaliza muda wake wa uwakilishi, hii ni ishara ya uhusiano wa karibu, undugu na urafiki uliopo baina ya Tanzania na Malawi,” amesema Balozi Mulamula

Kwa upande wake Balozi Mteule wa Malawi Mhe. Andrew Kumwenda amesema kuwa Malawi na Tanzania siku zote zimekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia na jukumu langu hapa kama Balozi ni kuhakikisha uhusiano huu unazidi kuku ana kuimarika.

“Tanzania inatekeleza Diplomasia ya Uchumi na vivyo hivyo Malawi………kwa hiyo sisi wote tuna lengo moja, na nitahakikisha Tanzania na Malawi zinashirikiana kufanya biashara na uwekezaji kwa maslahi ya pande mbili,” Amesema Balozi Kumwenda.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiongea na Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula mara baada ya kuwasilisha nakala ya Hati za Utambulisho 

Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda katika picha ya pamoja na maafisa walioambatana nao   



KAMATI YA KITAIFA YA KUZUIA MAUAJI YA KIMBARI YAJADILI MFUMO WA KUZUIA MIGOGORO NCHINI

$
0
0


 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene (katikati) akifungua  kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari kinachofanyika jijini Dar es Salaam kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na kushoto ni bibi Cristine Musisi Mwakilishi mkazi wa UNDP nchini 
 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari kinachofanyika jijini Dar es Salaam katikati ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene na kushoto ni bibi Cristine Musisi Mwakilishi mkazi wa UNDP nchini 


Mjwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari bibi Felistas Mushi akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Kamati hiyo kinachofanyika jijini Dar es Salaam

Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene (watatu kutoka kushoto waliokaa) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (watatu kutoka kulia waliokaa) baada ya kufunguliwa kwa kikao cha kamati yao kinachofanyika  Jijini Dar es Salaam kujadili uanzishwaji wa Mfumo wa kuzuia migogoro nchini


Na Mwandishi wetu, Dar es salaam

Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari imekutana Jijini Dar es Salaam kujadili uanzishwaji wa Mfumo wa kuzuia migogoro nchini ili kurahisisha shughuli za uratibu wa kamati hiyo.

Akifungua kikao cha kamati hiyo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. George Simbachawene amepongeza kuanzishwa kwa mfumo huo hapa nchini ambao utasaidia kutambua dalili za awali  katika matukio yanayoweza kusababisha kutokea mauaji ya kimbari.

“Naishukuru UNDP kwa kubuni wazo la kuanzishwa kwa mfumo huo, kwani kutambua dalili za awali za matukio yanayoweza kusababisha  kutokea kwa mauaji ya kimbari kutasaidia sana kuepusha kutokea kwa mauaji hayo siyo tu hapa nchini bali hata kwa nchi nyingine wanachama wa jumuiya yetu, ni wazo zuri na wadau wamelipokea vizuri,” amesema Mhe. Simbachawene.

Amesema Serikali inaendelea na taratibu za kuanzisha ofisi kwa ajili ya kuratibu mauaji ya kimbari hapa nchini kwa ajili ya kusaidia harakati za kuzuia kutokea kwa mauaji ya kimbari kupitia mfumo huo.

Kwa Upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameipongeza Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari ambayo imekuwa ikichukua hatua za kuwakutanisha wadau  mbalimbali katika jamii kama viongozi wa dini na jumuiya mbalimbali ili kutatua changamoto pale zinapotokea katika jamii nchini.

“Mimi kama mlezi wa kamati nimefarijika kuiona kamati hii ikitekeleza majukumu yake kwa ufanisi na siyo tu kuisaidia Tanzania bali hata nchi nyingine katika ukanda wa maziwa makuu,” amesema Balozi Mulamula.

Balozi Mulamula amepongeza Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kushirikiana na Serikali ya Uswisi kwa  kuona umuhimu wa Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari na hivyo kwa pamoja kuja na mpango wa kuanzishwa kwa kituo ambacho kitakuwa kinatoa taarifa za awali pale vinapokuwepo viashira vya matatizo au hata mauaji ya kimbari na kuongeza kuwa Serikali inaunga mkono jitihada hizo kwani zitaiwezesha kuzuia migogogo ambayo inaweza kusababisha kutokea mauaji  ya kimbari nchini.
  
Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari nchini iliundwa mwezi Februari, 2012 baada ya Tanzania kusaini na kuridhia Itifaki ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari iliyoridhiwa na Serikali ya Tanzania kupitia Mkataba wa nchi za Maziwa Makuu wa Usalama, Utulivu na Maendeleo.


WFP YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUBORESHA SEKTA YA KILIMO NCHINI

$
0
0

Na Mwandishi wetu, Dar 

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeahidi kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha kilimo nchini na kukifanya kuwa cha kisasa zaidi.

Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kanda ya Kusini mwa Afrika wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Dkt. Menghestab Haile alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Haile amesema WFP inajivunia uhusiano mzuri na Tanzania na itaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano huo kwa maslahi ya pande zote mbili.

“Leo tumejadili na kuona ni namna gani tunaweza kuwaunga mkono wakulima wa Tanzania ili waweze kupata faida zaidi kupitia kilimo ambapo faida hiyo itawasaidia kuyaboresha zaidi maisha yao,” amesema Dkt. Haile

“………… kwa kuwa kilimo ndiyo sekta pekee inayotoa fursa ya ajira kwa wingi duniani, tuna mkakati wa kuwawezesha vijana kujikita zaidi kwenye kilimo ili kupunguza tatizo la ajira,” amesema Dkt. Haile na kuongeza kuwa WFP itahakikisha Tanzania inakuwa kituo cha uzalishaji katika ukanda wa Kusini mwa Afrika kwa kuwa ina rasilimali za kutosha kuwekeza katika sekta ya Kilimo. 

Nae Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amemuahidi Mkurugenzi huyo wa WFP kuwa Serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha sekta ya kilimo nchini inaboreshwa zaidi.

“Nimewahakikishia WFP kuwa Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano katika kuhakikisha maboresho katika sekta ya kilimo yanafanyika na kuboresha maisha ya wakulima na kuwafanya vijana kujikita zaidi kwenye sekta hiyo muhimu,” amesema Balozi Mulamula.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na WFP katika kuboresha zaidi sekta ya kilimo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiongea na Mkurugenzi wa Kanda ya Kusini mwa Afrika wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Dkt. Menghestab Haile katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Kanda ya Kusini mwa Afrika wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Dkt. Menghestab Haile akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Mkurugenzi wa Kanda ya Kusini mwa Afrika wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Dkt. Menghestab Haile kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Mkurugenzi wa Kanda ya Kusini mwa Afrika wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Dkt. Menghestab Haile katika picha ya Pamoja Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bibi. Sarah Gordon-Gibson wa kwanza kushoto, kulia mwa Balozi Mulamula ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Makocha Tembele anayefuatia ni Bw. Hlalanathi Fundzo kutoka WFP.  





Balozi Possi Afanya Ziara ya Kikazi Jamhuri ya Czech

$
0
0

Balozi Possi Afanya Ziara ya Kikazi Jamhuri Czech

Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Czech mwenye makazi yake Berlin, Ujerumani, Dkt. Abdallah Possi amefanya ziara ya kikazi katika nchi ya Jamhuri ya Czech na kufanya mazungumzo na Naibu Mawaziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Miloslav Stašek; Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Jakub Dvořáček na Naibu Waziri wa Elimu, Mhe. Prof. Jaroslav Miller tarehe 17 Machi 2022.

Wakati wa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dkt. Possi aliwasilisha ombi ili Watanzania waweze kunufaika na Mpango wa Nafasi za Ufadhili wa Masomo unaoratibiwa na Wizara hiyo. Kwa sasa, nchi za Africa zinazonufaika na mpango huo ni Zambia na Ethiopia. Mhe, Naibu Waziri aliahidi kulifanyia kazi ombi hilo. Aidha, Mhe. Stašek aliwasilisha mualiko wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kufanya ziara ya kikazi Jamhuri ya Czech.

Katika mazungumzo yake na Naibu Waziri wa Afya, Balozi Possi aliomba Serikali ya nchi hiyo kuangalia uwezekano wa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika sekta ya Afya, hususan katika magonjwa ya moyo na figo. Serikali ya Jamhuri ya Czech imeahidi kulifanyia kazi ombi hilo na kuahidi pia kuwa ipo tayari kuisaidia Tanzania dozi za chanjo ya UVIKO-19.

Kwa upande wa mazungumzo na Naibu Waziri wa Elimu, wawili hao walijadili kuhusu ushirikiano wa Vyuo Vikuu, na namna ambavyo wanafunzi wa Tanzania waliokatiza masomo nchini Ukraine wanaweza kurahisishiwa mchakato wa kuhamisha alama na kumalizia masomo yao katika vyuo vikuu vya Czech.  Prof. Miller alimweleza Balozi Dkt. Possi wataanza na utaratibu wa awali wa kuvitaarifu vyuo vikuu vya Czech na kutoa kipaumbele kwa wanafunzi wa Tanzania, huku taratibu nyingine za kiufundi zikifuata.

Mhe. Miller aliahidi pia kuwa mamlaka husika zitaweka tangazo katika tovuti ya “Study in Czech Republic” ili  kuwahamasisha wanafunzi wa Tanzania waliokuwa Ukraine kuomba kujiunga na vyuo vikuu Jamhuri ya Czech.

 

Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Czech mwenye makazi yake Berlin, Ujerumani, Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Mhe.Miloslav Stašek walipokutana kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi zao.

Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Czech mwenye makazi yake Berlin, Ujerumani, Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na Naibu Waziri wa Elimu wa Jamhuri ya Czech,Mhe. Prof. Jaroslav Miller walipokutana kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya sekta za afya za nchi zao.

Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Czech mwenye makazi yake Berlin, Ujerumani, Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Jakub Dvořáček walipokutana kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya sekta za elimu za nchi zao.

 


 

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA DKT. STERGOMENA L. TAX AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA KAWAIDA WA SADC UNAOFANYIKA LILOLONGWE, MALAWI

$
0
0

   Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena L. Tax (Mb) akiongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa kawaida wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Lilongwe Malawi (Machi 18 – 19,2022). Kushoto kwa Dkt. Tax ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor (Mb) Mbarouk,akifuatiwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) na Mipango na Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb)


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena L. Tax (Mb) pamoja na ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alioongozana nao wakifuatilia Mkutano wa kawaida wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea Lilongwe,Malawi

    Sehemu ya Mawaziri wa Mawaziri wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika mkutano.


Mawaziri wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC )wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa kawaida wa Mawaziri wa SADC uofanyika Lilongwe Malawi Machi 18 – 19,2022

 

TANZANIA, EU ZAKUTANA KUJADILI EPA

$
0
0

Na Mwandishi wetu, Dar

Serikali ya Tanzania imekutana na Umoja wa Ulaya (EU) kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) kati ya Umoja huo na Tanzania.

Akiongea wakati wa kikao cha wataalamu kutoka Tanzania na EU kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara amesema kikao hicho kinalenga kujadili makubaliano yaliyokwama awali kutokana na Tanzania kutokuwa tayari kuridhia baadhi vipengele vilivyomo kwenye mkataba huo.

Prof. Kahyarara amesema Tanzania haikukubaliana na baadhi ya vipengele vya mkabata wa EPA na kuona kuwa ni vigumu kuingia katika makubaliano ya mkataba huo kabla ya kurekebisha vipengele hivyo.

“Tumekaa na wataalamu wetu na wenyewe wamekuja na wataalamu wao, tutapitia kipengele kimoja baada ya kingine na tunaamini tutafika mwisho na kama tulivyo waambia wenzetu wa EU tunaona faida ya kufanya biashara na wao kwa maslahi ya pande zote mbili,” amesema Prof. Kahyarara  

Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Mhe. Manfredo Fanti amesema majadiliano hayo yanalenga kuangalia vipengele vya mkataba ambavyo Tanzania ilionesha mashaka  katika kikao kilichopita ili kuvipatia ufumbuzi na kusonga mbele kwa pamoja hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania sasa inatoa kipaumbele katika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.

“Itakumbukwa kuwa Tanzania inatekeleza diplomasia ya uchumi na wawekezaji kutoka Umoja wa Ulaya wanania ya kuja kuwekeza Tanzania na Afrika Mashariki, hivyo tukikamilisha majadiliano haya itakuwa ni jambo lenye maslahi kwa pande zote,” Amesema Balozi Fanti.  

Kikao cha leo kinatokana na mazungumzo ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyafanya alipokuwa katika ziara ya kikazi nchini Ubelgiji ambapo alikutana na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Ulaya, Bw. Charles Michael mwezi Februari 2022.

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Mhe. Manfredo Fanti akiongea na washiriki wa kikao (hawapo pichani), kulia ni Katibu Mkuu wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara katika kikao kilichofanyika Jijini Dar es Salaam


Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Mhe. Manfredo Fanti akiongea na washiriki wa kikao, kulia ni Katibu Mkuu wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara katika kikao kilichofanyika Jijini Dar es Salaam


Kikao kikiendelea 

Washiriki kutoka Tanzania na Umoja wa Ulaya wakiwa katika picha ya pamoja


MKUTANO WA 15 WA BARAZA LA KISEKTA LA KILIMO NA USALAMA WA CHAKULA KUFANYIKA DAR ES SALAAM

$
0
0

Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Maafisa Waandamizi umeanza kufanyika leo tarehe 21 Machi 2021 katika Hoteli ya Four Points, jijini Dar es Salaam. Mkutano huu wa siku tano (5) utakaofanyika kwa njia ya mseto (video na ana kwa ana) kuanzia tarehe 21 hadi 25 Machi 2022, unatarajiwa kuangazia masuala mbalimbali katika sekta ya kilimo yanayolenga kuhakikisha maendeleo endelevu katika sekta ya kilimo na usalama wa chakula ndani ya Jumuiya. 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano huo Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Sekta za Uzalishaji na Huduma za Jamii katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Christophe Bazivamo alibainisha umuhimu wa Mkutano huo kuangazia maeneo ya msingi ambayo yakifanyiwa kazi na nchi wanachama, Jumuiya itafikia lengo la kuwa na maendeleo endelevu katika sekta ya kilimo na usalama wa chakula. Ameyataja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni; kuweka na kutekeleza mikakati ya kuboresha miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji, kuwawezesha na kuwahimiza wanawake na vijana kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye sekta ya kilimo na kuhimiza matumizi ya teknolojia ya kisasa kwenye kilimo ili kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao.

“Nimatumaini yangu haya machache niliyo yabainisha hapa, na mengi ya muhimu ambayo wataalamu mtajadili kwa kina katika mkutano huu yatachangia kwa kiasi kikubwa kuchochea kasi ya ukuaji wa kilimo na kuleta mabadiliko chanya katika ustawi wa pamoja na kuboresha maisha Wanaafrika Mashariki” alisema Bw. Bazivamo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mkutano huo Dkt. Mary Mwale kutoka Jamhuri ya Kenya akirejea takwimu zilizotolewa na Ripoti ya tatu ya Mpango Kamili wa Maendeleo ya Kilimo Afrika (Comprehensive Africa Agriculture Development Programme - CAADP) ya mwaka 2022 amewahimiza wataalamu wa kilimo katika Jumuiya kuzisaidia Serikali kuongeza nguvu na ubunifu katika kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo ambayo imeajiri asilimia 80 ya Idadi ya watu wote katika Jumuiya. 

Ripoti ya miaka mitatu ya CAADP iliyotolewa mwezi Machi 2022 imebainisha kuwa ukanda wa Afrika Mashariki isipokuwa Jamhuri ya Rwanda hazikufikia malengo yaliyoafikiwa kwenye mpango wa Afrika wa kufikia mabadiliko ya kilimo, uzalishaji mali, usalama wa chakula na lishe, ukuaji wa uchumi, na ustawi kwa wote. 

Jumuiya tuna kazi kubwa ya kufanya kwenye Sekta ya Kilimo, tunawajibu mkubwa wa kuhakikisha maendeleo ya kilimo yanakuwa endelevu na yenye tija ni muhimu pia kukumbuka kuwa 70% ya viwanda vya Jumuiya ya Afrika Mashariki vinategemea sekta ya kilimo, vikiwemo vya uzalishaji wa pembejeo za kilimo; wakati huo huo 65% ya bidhaa zinazouzwa katika Jumuiya zinatokana na kilimo na bidhaa za kilimo. alisema Dkt. Mwale

Mkutano huu wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utafanyika katika ngazi tatu; ngazi ya Wataalamu Waandamizi tarehe 21 na 23 Machi, Ngazi ya Makatibu Wakuu tarehe 24 Machi, na mwisho ngazi ya Mawaziri tarehe 25 Machi 2022. 

Mkutano huu umehudhuriwa na nchi zote sita (6) wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) Bw. Patrick Gwediagi (wakwanza kushoto) ambaye pia ni Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ngazi ya Wataalamu Waandamizi akifuatilia Mkutano huouliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Sekta za Uzalishaji na Huduma za Jamii katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Christophe Bazivamo akifungua Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam.
Meza kuu wakifuatilia Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam.
Bw. Hassan Mnondwa Afisa Biashara katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa kwenye Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam.
 Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam
Dkt. Mary Mwale kutoka Jamhuri ya Kenya akiongoza Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam.
Viewing all 3230 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>