EMPLOYMENT OPPORTUNITIES
Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE atembelea Banda la Tanzania, Dubai
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Sheikh Abdullah bin Zayed tarehe 13 februari 2022 ametembelea Banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Expo 2020 Dubai na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Mohamed Abdullah Mtonga ambaye pia ni Kamishna Jenerali wa Banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Expo 2020 Dubai.
Baada ya kuwasili kwenye banda hilo na kutembezwa, Mhe. Zayed aliipongeza Tanzania kwa kuandaa Banda lenye mvuto na linaloonyesha vivutio vya utalii pamoja na fursa zilizopo katika sekta mbalimbali kama za utalii, nishati, uchukuzi na madini.
Kwa upande wake, Mhe. Balozi alimshukuru Mgeni wake kwa kuchagua kutembelea banda la Tanzania ikiwa ni moja ya nchi 192 zinazoshiriki maonesho hayo. Aidha, aliishukuru Serikali ya UAE kwa kuandaa vizuri Maonesho makubwa ya Expo 2020 Dubai, licha ya uwepo wa changamoto ya kuenea kwa ugonjwa wa COVID -19.
Ushiriki wa Tanzania unatarajiwa kuwa na matokeo chanya na kuongeza idadi ya Watalii watakaoitembelea Tanzania, wawekezaji, mitaji pamoja na masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini. Katika Maonesho haya, Tanzania ni miongoni mwa nchi 50 ambapo kwa mara ya kwanza zinashiriki kwenye mabanda pekee yaliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya UAE.
Katika hatua nyingine, Ubalozi wa Tanzania, UAE utasherehekea Siku ya Kitaifa (National Day) tarehe 27 Februari 2022. Sherehe hizo zitapambwa na shughuli mbalimbali zikiwemo Kongamano kubwa la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Ballon, Hoteli ya Jumeirah Beach tarehe 27 Februari 2022.
=====================================================================
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Sheikh Abdullah bin Zayed akiangalia miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa nchini inayooneshwa kwenye Banda la Tanzania katika Maonesho ya Expo 2020 Dubai. |
Balozi Mbega Awasilisha Hati za Utambulisho, India
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa K. Mbega amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa India, Mhe. Ram Nath Kovind , Ikulu (Rashtrapati Bhavan), mjini New Delhi leo tarehe 16 Februari 2022. Baada ya kuwasilisha Hati hizo, Balozi Anisa Mbega alifanya mazungumzo na Mhe. Rais Kovind. Wakati wa mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Balozi Anisa Mbega aliishurukuru Serikali ya India kwa misaada mbambali wanayoipatia Tanzania hususan, mikopo ya masharti nafuu katika sekta ya maji pamoja na misaada mbalimbali kama vile madawa na vifaa tiba pamoja na nafasi za mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa watanzania. Aidha, alimpa Mhe. Rais Kovind salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suhuhu Hassan ambapo Mhe. Rais Kovind alishukuru kwa salamu hizo. Vilevile, Mhe. Balozi Anisa Mbega aliahidi kuwa Tanzania itaendelea kudumisha uhusiano uliopo wa muda mrefu katika nyanja mbalimbali ikiwemo biashara, uwekezaji, utalii na pia kufungua milango ya ushirikiano katika maeneo mengine. Rais Kovind alisifu uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na India na akasisitiza kuwa India itaendelea kushirikiana na Tanzania kwenye nyanja mbalimbali. Aidha, alimuhakikishia Balozi Anisa Mbega kuwa Serikali ya India ipo tayari kutoa ushirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa wepesi na ufanisi kwa maslahi ya wananchi wa pande zote. |
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa .K. Mbega akisalimiana na Rais wa India, Mhe. Ram Nath Kovind alipowasili kwenye Ikulu ya Rashtrapati Bhavan jijini New Delhi kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. |
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa K. Mbega akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa India, Mhe. Ram Nath Kovind , Ikulu (Rashtrapati Bhavan), jijini New Delhi |
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa K. Mbega akiwa katika mazungumzo na Rais wa India, Mhe. Ram Nath Kovind kwenye Ikulu ya Rashtrapati Bhavan jijini New Delhi baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. |
FURASA ZA KAZI NA UFADHILI WA MASOMO
BALOZI MBAROUK AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUMUAGA BALOZI EDWIN RUTAGERUKA
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akiongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasi ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Marehemu Balozi Edwin Rutageruka katika kijiji cha Musibuka, Wilayani Misenyi Mkoani Kagera.
Sehemu ya Waombolezaji wakiwa msibani |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) pamoja na mume wake wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Balozi Edwin Rutageruka |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiweka taji kwenye kaburi la Balozi Edwin Rutageruka |
Wanadiaspora Wahamasishwa Kutumia Bidhaa zinazobuniwa kwa ajili yao.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Tagie Daisy Mwakawago akisaini Kitabu cha Wageni kwenye Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar Es Salaam. Bi. Mwakawago alitembelea benki hiyo kujadili na uongozi kuhusu unazishwaji wa bidhaa mpya kwa ajili ya diaspora na maendeleo ya matumizi ya bidhaa zilizopo kwa wanadiaspora. |
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Tagie Daisy Mwakawago (aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa benki ya NMB baada ya kufanya mazungumzo na watumishgi hao. |
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Tagie Daisy Mwakawago akiwa na mmiliki wa Hamidu City Park, Bw. Hamidu Mvungi. Hamidu City Park ni mradi wa nyumba uliopo Kigamboni jijini Dar Es Salaam ambao Kaimu Mkurugenzi ameenda kuuona ili kujiridhisha kwa ajili ya kuwahamasisha wanadiaspora kununua nyumba kwenye mji huo. |
Sehemu ya nyumba zinavyoonekana kwenye mji huo. |
INVITATION FOR TENDERS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND EAST AFRICAN COOPERATION
Tender No. ME- 013/2021- 2022/HQ/W/01
For
PROPOSED CONSTRUCTION OF CHANCERY AND INVESTMENT BUILDING FOR THE TANZANIA EMBASSY IN KINSHASA, DRC.
Invitation for Tenders
Date: 15th February, 2022
1 This Invitation for Tenders follows the General Procurement Notice (GPN) for this Project on 24thSeptember, 2021.
2 The Government of the United Republic of Tanzania has set aside funds for the operation of the Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation during the financial year 2021/2022. It is intended that part of the proceeds of the fund will be used to cover eligible payment under the contract for ProposedConstruction of Chancery and investment building for the Tanzania Embassy in Kinshasa, DRC.
3 The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation now invites sealed Tenders from eligible contractors registered in NCA CLASS I (NCA1) CLASS I (ONE) CATEGORY for carrying out of the Proposed Construction of Chancery and Investment Building for the Tanzania Embassy in Kinshasa, DRC.
4 Tendering will be conducted through INTERNATIONAL COMPETITIVE TENDERING as specified in the Public Procurement Regulations, Government Notice No.446 of 2013 and is open to all Tenderers as defined in the Regulations unless otherwise stated in the Tender Data Sheet.
5 Interested eligible Tenderers may obtain further information and inspect the Tendering Documents from Tanzania Electronic Procurement System (TANePS). www.taneps.go.tz
6 All Tenders must be accompanied by Tender security of 2% of the tender value in the format provided in the Tender documents unless stated in the Tender Data sheet. The tender Security in the original form shall be submitted to the Director of Procurement Management Unit, Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation, Office, 6th Floor PSSSF House Makole Street Dodoma City, Tanzania before the deadline indicated on para 7 below.
7 All Tenders must be submitted in the proper format, at or before on 10th March, 2022.Tenders will be promptly thereafter opened upon the presence of Bidder’s Representative who wish to attend TANeps on or before 13:00 Hours EAT Thursday hours on the 10th March, 2022. Tenders will be opened promptly thereafter in public and in the presence of Tenderers’ Representatives who choose to attend.
8 Late Tenders, not submitted online through TANePs and Tenders not opened electronically through on the Tender opening day and time shall not be accepted for evaluation irrespective of the circumstances.
PERMANENT SECRETARY
MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND EAST AFRICAN COOPERATION,
Government City
Mtumba Area,
P.O Box 2933, 40466 Dodoma
*********************************************************************************************************
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND EAST AFRICAN COOPERATION
Tender No. ME-013/2020-2021/HQ/W/02
For
THE CONSTRUCTION OF THE PROPOSED CHANCERY AND AMBASSADOR’S RESIDENCE BUILDINGS IN TANZANIA EMBASSY MUSCAT OMAN
Invitation for Tenders
Date: 15th February, 2022
1 This Invitation for Tenders follows the General Procurement Notice (GPN) for this Project on 24thSeptember, 2021.
2 The Government of the United Republic of Tanzania has set aside funds for the operation of the Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation during the financial year 2021/2022. It is intended that part of the proceeds of the fund will be used to cover eligible payment under the contract for The Construction of the Proposed Chancery and Ambassador’s Residence Buildings in Tanzania Embassy Muscat, Oman.
3 The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation now invites sealed Tenders from eligible contractors registered in CLASS I (ONE) CATEGORY for carrying out of the Proposed Chancery and Ambassador’s Residence Buildings in Tanzania Embassy Muscat, Oman.
4 Tendering will be conducted through NATIONAL COMPETITIVE TENDERING as specified in the Public Procurement Regulations, Government Notice No.446 of 2013 and is open to all Tenderers as defined in the Regulations unless otherwise stated in the Tender Data Sheet.
5 Interested eligible Tenderers may obtain further information and inspect the Tendering Documents from Tanzania Electronic Procurement System (TANePS). www.taneps.go.tz
6 All Tenders must be accompanied by Tender security of a ‘’minimum of 2 percent,’’of the bid price or an equivalent amount in a freely convertible currency in the form of Unconditional Bank Guarantee as provided in the Tendering documents.
7 All Tenders properly filled in must be submitted in TANeps on or before 13:00 Hours EAT Thursdayhours on the 10th March, 2022. Tenders will be opened promptly thereafter in public and in the presence of Tenderers’ Representatives who choose to attend in the opening at 6th Floor, PSSSF House, Makole Street, Director of Procurement Management Unit Office.
8 Late Tenders, Portion of Tenders, electronic Tenders, Tenders not received. Tenders not opened at the Tender opening ceremony shall not be accepted for evaluation irrespective of the circumstances.
PERMANENT SECRETARY
MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND EAST AFRICAN COOPERATION,
Government City
Mtumba Area,
P.O Box 2933, 40466 Dodoma
***************************************************************************************************
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND EAST AFRICAN COOPERATION
Tender No. ME-013/2020-2021/HQ/W/02
For
THE CONSTRUCTION OF THE PROPOSED CHANCERY AND INVESTMENT BUILDING FOR THE TANZANIA HIGH COMMISSION IN NAIROBI, KENYA
Invitation for Tenders
Date: 15th February, 2022
1 This Invitation for Tenders follows the General Procurement Notice (GPN) for this Project on 24thSeptember,2021.
2 The Government of the United Republic of Tanzania has set aside funds for the operation of the Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation during the financial year 2021/2022. It is intended that part of the proceeds of the fund will be used to cover eligible payment under the contract for the THE CONSTRUCTION OF THE PROPOSED CHANCERY AND INVESTMENT BUILDING FOR THE TANZANIA HIGH COMMISSION IN NAIROBI, KENYA.
3 The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation now invites sealed Tenders from eligible contractors registered in NCA CLASS I (NCA 1) Category for carrying out of the Proposed Construction of Chancery and nvestment Building For The Tanzania High Commission in Nairobi, Kenya.
4 Tendering will be conducted through International Competitive Tendering as specified in the Public Procurement Regulations, Government Notice No.446 of 2013 and is open to all Tenderers as defined in the Regulations unless otherwise stated in the Tender Data Sheet.
5 Interested eligible Tenderers may obtain further information and inspect the Tendering Documents from Tanzania Electronic Procurement System (TANePS). www.taneps.go.tz
6 All Tenders must be accompanied with Tender security of 2% of the tender value in the format provided in the Tendering documents unless otherwise stated in the Tender Data Sheet. The Tender Security in the original form shall be submitted to the Director Procurement Management Unit, Director, Procurement Management Unit, Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation, Office, 6th Floor PSSSF House Makole Street Dodoma City, Tanzania before the deadline indicated on Para 7 below.
7 All Tenders must be submitted in the proper format, at or before 11:30 Hours EAT on 10th March, 2022. Tenders will be promptly thereafter opened upon the presence of Bidder’s Representative who wish to attend.
8 Late Tenders not submitted online through TANePS and Tenders not opened electronically through TANePS on the Tender opening day and time shall not be accepted for evaluation irrespective of the circumstances.
PERMANENT SECRETARY
MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND EAST AFRICAN COOPERATION,
Government City
Mtumba Area,
P.O Box 2933, 40466 Dodoma
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND EAST AFRICAN COOPERATION
Tender No. ME- 013/2020-2021/HQ/W/04
For
THE PROPOSED REHABILITATION WORKS FOR TANZANIA’S OLD CHANCERY BUILDING ALONG 2139 R- STREET NM WASHNGTON, DC 20008 USA
Invitation for Tenders
Date: 15th February, 2022
1 This Invitation for Tenders follows the General Procurement Notice (GPN) for this Project on 24thSeptember, 2021.
2 The Government of the United Republic of Tanzania has set aside funds for the operation of the MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND EAST AFRICAN COOPERATION during the financial year 2021/2022. It is intended that part of the proceeds of the fund will be used to cover eligible payment under The Proposed Rehabilitation Works for Tanzanian’s Old Chancery Building along 2139 R-Street NW Washington,DC 20008 USA
3 The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation now invites sealed Tenders from eligible contractors registered in CLASS I CATEGORY for carrying out The Proposed Rehabilitation Works for Tanzanian’s Old Chancery Building along 2139 R-Street NW Washington, DC 20008 USA.
4 Tendering will be conducted through NATIONAL COMPETITIVE TENDERING as specified in the Public Procurement Regulations, Government Notice No.446 of 2013 and is open to all Tenderers as defined in the Regulations unless otherwise stated in the Tender Data Sheet.
5 Interested eligible Tenderers may obtain further information and inspect the Tendering Documents from Tanzania Electronic Procurement System (TANePS). www.taneps.go.tz
6 All Tenders must be accompanied with Tender security of 2% of the tender value in the format provided in the Tendering documents unless otherwise stated in the Tender Data Sheet. The Tender Security in the original form shall be submitted to the Director Procurement Management Unit, Director, Procurement Management Unit, Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation, Office, 6th Floor PSSSF House Makole Street Dodoma City, Tanzania before the deadline indicated on Para 7 below.
7 All Tenders must be submitted in the proper format, at or before 12:30 Hours EAT on 10th March, 2022. Tenders will be promptly thereafter opened upon the presence of Bidder’s Representative who wish to attend.
8 Late Tenders portion of Tenders, electronic Tenders, Tenders not received, Tenders not opened at the Tender opening ceremony shall not be accepted for evaluation irrespective of the circumstances.
PERMANENT SECRETARY
MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND EAST AFRICAN COOPERATION,
Government City
Mtumba Area,
P.O Box 2933, 40466 Dodoma
FURSA ZA MASOMO
BALOZI MBAROUK AMUAGA BALOZI WA VATICAN
Na Mwandishi wetu, Dar
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) amekutana na kumuaga Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczyński baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.
Akiongea wakati wa kumuaga Balozi wa Vatican jana jioni katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam, Balozi Mbarouk amempongeza Balozi Solczyński kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Tanzania.
Pamoja na mambo mengine, Balozi Mbarouk amemuahidi Askofu Mkuu Solczyński kuwa Tanzania na Vatican zitaendelea kuhimiza amani na utulivu katika masuala yenye changamoto mbalimbali ili kuwezesha uwepo wa amani na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Baba Mtakatifu katika kulinda Amani na usalama duniani kote.
Kwa upande wake Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Marek Solczynski, amesema kuwa Vatican itaendelea kuimarisha mahusiano yake ya kidiplomasia na Tanzania kwa masuala yenye maslahi ya amani na utulivu pamoja na haki na utu.
“Tumeongelea masuala mbalimbali katika kukuza diplomasia yetu na tumekubaliana kwa pamoja kudumisha amani na usalama duniani ili kuweza kuchagiza maendeleo endelevu kwa pande zote mbili,” amesema Askofu Mkuu Solczynski.
Balozi wa Vatican nchini Askofu Mkuu Marek Solczyński aliwasili nchini Tanzania Julai 12, 2017.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimkabidhi Balozi wa Vatican nchini Mhe. Askofu Mkuu Marek Solczyński zawadi ya kinyago
TAARIFA KUHUSU WATANZANIA WANAOISHI UKRAINE
BALOZI KOMBO AKUTANA NA WADAU WA NGO’s JIJINI ROMA
Na Mwandishi wetu, Roma
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amekutana na kufanya mkutano na wadau wa NGO’s takribani sitini na nne zinazofanya shughuli zake nchini Tanzania mwishoni mwa wiki Jijini Roma, Italia.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na wadau mbalimbali wa Diaspora pamoja na wadau wa NGO walimpongeza Mhe. Balozi kwa kuwapa nafasi ya kujitambulisha na kutoa fursa ya kuwasikiliza mafanikio yao sambamba na changamoto wanazopitia katika kufanikisha shughulika zao nchini Tanzania.
Pamoja na kuwasikiliza lakini pia Balozi alitumia nafasi hiyo kuwashauri kuwa na ushirikiano wa pamoja ili kuleta ufanisi zaidi kwenye maeneo wanayo yafanyia kazi. Aidha, katika mkutano huo Balozi Kombo aliongea mubashara na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Marco Lombardi na kumpa fursa ya kutoa salaam zake moja kwa moja kwa njia ya mtandao.
Balozi wa Italia nchini Tanzania aliwahakikishia wadau hao kuwa wapo kwenye mikono salama ya Balozi wa Tanzania Rome na chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Tanzania ni nchi salama ya kufanya shughuli zao.
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa mmoja wa wadau wa NGO's mwishoni mwa wiki Jijini Roma, Italia Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akipokea akiwa katika kikao na wadau wa NGO's mwishoni mwa wiki Jijini Roma, Italia
Denmark na Tanzania zaahidi kuimarisha Ushirikiano
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan imejipambanua kuwa imedhamiria kuboresha mazingira ili kutoa fursa kwa wadau kushiriki katika sekta mbalimbali, iwe siasa, biashara, uwekezaji au masuala ya usawa wa kijinsia.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) alipokutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Denmark anayehusika na Masuala ya Sera na Maendeleo, Bi. Lotte Machon jijini Dar Es Salaam tarehe 28 Februari 2022.
Balozi Mulamula alieleza kuwa tokea Rais Samia aingie madarakani Serikali yake imechukua hatua mbalimbali za kuboreha mazingira ya biashara na uwekezaji, kutoa uhuru zaidi wa kisiasa, kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kuimarisha ushirikiano na nchi za nje na mashirika ya kimataifa, kuboresha miundombinu na kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO-19.
Balozi Mulamula alieleza kuwa ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Denmark umetimiza miaka 60 sasa, na katika kipindi hicho, nchi hizo mbili zimeshirikiana katika maeneo mengi ikiwemo Tanzania kufaidika na misaada ya Denmark katika sekta tofauti kama vile; huduma za afya, elimu, mabadiliko ya mifumo ya kodi, nishati, kilimo, athari za mabadiliko ya tabianchi, biashara na uwekezaji.
Mhe. Waziri alimuhakikishia Bi. Machon kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Denmark na kusisitiza umuhimu wa nchi hiyo kuendelea kuisaidia Tanzania hususan, kwa kuunga mkono jitihada za kuhamasisha wawekezaji wengi zaidi wa Denmark kuja kuwekeza nchini ili pamoja na mambo mengine uwekezaji huo uweze kutoa ajira kwa vijana ambao idadi yao kwa nchi za Afrika ni kubwa.
Kwa upande wake, Bi. Machon alielezea utayari wa Denmark kuendelea kushirikiana na Tanzania kwenye maeneo tofauti yakiwemo ya demokrasia, nishati na mabadiliko ya tabianchi. Alisema nchi hiyo kila mwaka inatenga asilimia 1 ya pato lake kwa ajili ya misaada ya maendeleo kwa nchi marafiki ikiwemo Tanzania.
Ujumbe aliongozana nao Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Denmark anayehusika na Sera na Maendeleo, Bi. Lotte Machon ukinukuu dondoo muhimu za mazungumzo. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akitoa maelezo ya zawadi aliyomkabidhi Katibu Mkuu wa Denmark. |
SADC Yazindua Kituo cha Ugaidi Dar Es Salaam
Waziri wa Kazi, Ajira, Tija, na Ukuzaji wa Ujuzi wa Botswana, Mhe. Machana Ronald Shamukuni, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Mhe. Maledi Pandor akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Kupambana na Ugaidi cha SADC jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali walioshiriki hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Kupambana na Ugaidi cha SADC |
TANZANIA , UNHCR WAKUTANA DAR ES SALAAM
1. Washiriki wa mkutano wa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) wakifuatilia mkutano huo unaofanyika jijiini Dar es Salaam |
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) wanakutana jijini Dar es Salaam kujadili utekelezaji wa majukumu ya kuwahudumia wakimbizi nchini na kuimarish ushirikiano kati ya pande mbili.
Mkutano huo wa majadiliano unafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 01 hadi 02 Machi 2022 unatokana na mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Kamishina Mkuu wa UNHCR, Bw. Filippo Grandi yaliyofanyika New York, Marekani mwezi Septemba 2021.
Mkutano huo umefunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni (Mb) na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi wa Serikali ya Tanzania na UNHCR akiwemo Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Bw. Christopher Kadio.
Akifungua mkutano huo Mhe. Waziri Masauni aliihakikishia Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania itaendelea kuheshimu haki za wakimbizi kwa kuzingatia sheria za kimataifa na bila kusahau sheria za nchi.
Waziri Masauni amesisitiza umuhimu wa wadau kutoa misaada kwa ajili ya kuboresha huduma na miundombinu ya kuwahudumia wakimbizi pamoja na jamii inayozuunguka makambi ambayo kwa kawaida huwa inaathirika kutokana na ongezeko la watu.
Mhe. Masauni amesema zoezi la kuwarejesha wakimbizi ni la hiyari na linafanyika kufuatia hali ya usalama nchini Burundi kuimarika.
Akizungumza katika kikao hicho Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) ambaye anaongoza majadiliano hayo amesema historia ya Tanzania ya kupokea na kuhifadhi wakimbizi sio ya kutiliwa shaka.
Amesema jukumu hilo limekuwa ni moja ya sera ya nchi na kusisitiza umuhimu wa UNHCR na Serikali kuimarisha ushirikiano ili kuendelea kutimiza jukumu hilo la kibinadamu kwa mafanikio makubwa, kwa sababu suala la wakimbizi halitarajiwi kumalizika katika kipindi kifupi kijacho.
Nao viongozi wa UNHCR wanaoshiriki Mkutano huo wakiongozwa na Kamishina Msaidizi wa Hifadhi, Bibi. Gillian Triggs na Kamishina Msaidizi wa Uendeshaji Bw. Raouf Mazou, Mratibu Mkazi wa UNHCR nchini, Bw. Ziatan Milisic wameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kupokea na kuwahifadhi wakimbizi.
Walisema Tanzania imekuwa ikipokea wakimbizi tokea miaka mingi iliyopita na hadi sasa kuna wakimbizi 147,000 nchini ambao wamekuwa wakipatiwa huduma stahiki na hadi wengine, 162,000 kutoka Burundi kupatiwa uraia.
Viongozi hao walielezea miradi mbalimbali inayotekelezwa na inayotarajiwa kutekelezwa na wadau kwa ajili ya kuboresha maisha ya waimbizi na jamii inayowazunguka. Miradi hiyo imejikita katika utoaji wa elimu bora, utunzaji wa mazingira, kuwajengea uwezo vijana na wanawake pamoja na kuboresha huduma mbalimbali kwa jamii zinazoishi karibu na makambi.
Walisema katika miaka ya karibuni UNHCR imetumia Dola za Marekani milioni 1.3 kwa ajili ya kuimarisha huduma mbalimbali ikiwemo usalama mkoani Kigoma.
Mkutano huo wa majadiliano ya ngazi ya juu unajadili ajenda za hifadhi ya ukimbizi, na jitihada za serikali za kuhudumia wakimbizi, kinga , haki na mahusiano ya kiutendaji kati ya Serikali na UNHCR.
RAIS WA TCCIA NCHINI AFANYA ZIARA YA KIKAZI OMAN
Rais wa Chama Cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima Tanzania (TCCIA), Bw. Paul Faraji Koyi, amefanya ziara ya kikazi nchini Oman hivi karibuni. Akiwa nchini Oman amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na wenye Viwanda ya Oman,
Katika mazungumzo yao, ambayo yalihudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Abasi Kilima, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo kukuza biashara na uwekezaji baina ya pande hizo mbili ili kuzitumia kikamilifu fursa nyingi za kiuchumi zinazopatikana katika nchi hizi mbili na hatimaye kukuza kiwango cha biashara kati ya nchi hizi ambacho kwa sasa kinaonekana bado kipo chini.
Wakati wa mazungumzo hayo, Bw. Koyi aliueleza ujumbe wa Oman kuwa, zipo fursa nyingi nchini Tanzania ambazo Oman inaweza kunufaika nazo zikiwemo za uwekezaji wa Viwanda vya kuchakata mazao ya Kilimo, Utalii, Uzalishaji Umeme, Kilimo, Ujenzi wa nyumba na sekta ya usafirishaji wa anga na baharini. Kadhalika aliwajulisha kuwa, Serikali ya Tanzania inachukua hatua mbalimbali za kuboresha miundombinu ya umeme, barabara, reli na viwanja vya ndege Ili kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara.
Kwa upande wake, Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Oman, Mhandisi Al Saleh aliwaeleza wajumbe kuwa, nchi hiyo imefungua milango ya uwekezaji katika Maeneo Huru ya Uwekezaji (EPZ) ya Salala, Duqm na Sohar. Aidha, Serikali ya Oman imetoa fursa kwa wawekezaji kutoka nje kutolazimika kuwa na ubia na mwekezaji mwenyeji.
Akizungumzia suluhisho la changamoto za ufanyaji biashara kati ya Tanzania na Oman, Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdalah Kilima amesema tayari Ubalozi huo umewasilisha pendekezo hapa nchini la kuanzisha safari za ndege ya mizigo kwenda Oman kupitia Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL). Pia Ubalozi umezungumza na mashirika ya meli nchini Oman ili kuanzisha safari za moja kwa moja kati ya nchi hizi mbili
Wakati huohuo, Ujumbe wa Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Wakulima ya Tanzania walikutana na Viongozi wa Baraza la Biashara kati ya Oman na Tanzania wa upande wa Oman ambapo walikubaliana kufufua mikakati ya ushirikiano kupitia Kampuni ya Uwekezaji ya Oman na Tanzania (OTIC) iliyoanzishwa mwaka 2016.
Mbali na kushiriki mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Oman, Ujumbe wa TCCIA ulifanya ziara katika Kiwanda cha Taifa cha Chai cha Oman, wazalishaji wa chai ya MUMTAZ jijini Muscat na kupata maelezo ya utendaji wa kiwanda hicho ambapo pamoja na mambo mengine, Kampuni hiyo imeahidi kufuatilia fursa zilizopo nchini, ikiwemo upatikanaji wa chai.
Kwenye ziara hiyo, Rais wa TCCIA nchini alifuatana na Bw. Abdul Mwilima, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Kigoma; Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Nerbat Mwapele na Afisa Masoko Mwandamizi, Bi. Fatma Khamis.
TANZANIA IRELAND KUENDELEZA USHIRIKIANO
Balozi wa Ireland nchini Mhe. Mary O’Neil akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mtakatifu Patrick zilizofanyika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania walioshiriki sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mtakatifu Patrick zilizofanyika nyumbani kwa Balozi wa Jamhuri ya Ireland jijini Dar es Salaam. |
Tanzania na Ireland zimeahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo kwa manuufaa ya pande zote mbili
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) ametoa ahadi hiyo aliposhiriki katika maadhimisho ya Siku ya Mtakatifu Patrick ambayo huadhimishwa na Jamhuri ya Ireland tarehe 17 ya kila mwaka.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku hiyo Waziri wa Mulamula ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Ireland kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo wa Tanzania hasa katika Nyanja za kusaidia kaya masikini, elimu na kuwajengea uwezo wanawake na watoto wa kike nchini.
Amesema Serikali inathamini mchango wa Ireland kwa Tanzania na kusisitiza kuwa itaendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo ili kufikia maendeleo ya kweli kwa pamoja.
Naye Balozi wa Ireland nchini Mhe. Mary O’Neil ameahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada za kuwaletea wananchi wake maendeleo.
Amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Ireland na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo kwa faida ya wananchi wa nchi zote.
Maadhimisho ya siku hiyo yamezinduliwa rasmi leo Tarehe 02 Machi 2022 jijini Dar es Salaam katika makazi ya Balozi wa Ireland nchini na kuhudhuriwa na Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi za Kimataifa wanaoziwakilisha nchi na Mashirika yao hapa nchini.
Siku ya Mtakatifu Patrick huadhimishwa kila ifikapo tarehe 17 Machi nchini Ireland kuadhimisha kuwasili kwa ukristo nchini humo na kusherehekea urithi wa utamaduni wa watu wa Ireland kwa ujumla.
WAZIRI MULAMULA AZINDUA BARAZA LA UONGOZI LA CHUO CHA DIPLOMASIA
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Diplomasia (CFR) wakimsikiliza Waziri Mulamula wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Diplomasia (CFR) wakimsikiliza Waziri Mulamula wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo jijini Dar es Salaam. |
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha CFR Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi akizungumza neno la shukurani kwa Mhe. Waziri Mulamula baada ya uzinduzi wa Baraza la Chuo hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amezindua Baraza la Uongozi la Chuo cha Diplomasia (CFR) na kuwataka wajumbe wa Baraza hilo kufanya mabadiliko katika uendeshji wa Chuo hicho huku wakizangatia muktadha wa uanzishwaji wake
Balozi Mulamula amewataka wajumbe wa baraza hilo kuwasiliana na mamlaka husika ili CFR ibaki katika muundo wake wa asili yakiwemo maudhui ya kuanzishwa kwa chuo hicho ili kutojitenga kabisa na kuktadha huo huku kikiangalia namna bora ya kujiendesha.
“leo hii tuko hapa kuzindua Baraza la Chuo, Mwenyekiti na wajumbe wa Baraza hili, naomba muwasiliane na Mamlaka husika ili kuona namna Chuo kitakavyoweza kuendelea kufuata na kutekeleza nia na madhumuni ya kuanzishwa kwake na huku mkiangalia namna ya kujiendesha,”alisema Balozi Mulamula.
Amesema pamoja na kuwa Chuo kinaangalia namna mbalimbali za kujiendesha lakini hakiondoi jukumu lake la asili ambalo lililenga kuanzishwa kwake.
Amelitaka Baraza hilo kuangalia upya na kuandaa kozi mbalimbali ambazo walikuwa wakipatiwa maafisa mambo ya nje ili kuwawezesha maafisa hao kwenda na wakati na kuongeza ujuzi.
Akizungumza katia uzinduzi huo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine amesema Uteuzi wa wajumbe wa Baraza hilo la Chuo utasaidia Chuo katika utekelezaji wa majukumu yake hasa ikizingatiwa sifa za wajumbe wa baraza hilo.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi amemuhakikishia Mhe. Waziri utayari wa wajumbe wa baraza hilo katika kutekeleza majukumu yake ili kukifanya chuo hicho kutimiza malengo yake.
WIZARA YAKABIDHI OFISI KWA CHAMA CHA MABALOZI WASTAAFU NCHINI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Mabalozi Wastaafu nchni na baadhi ya viongozi wa Wizara wakati wa hafla ya kukabiddhiwa Ofisi kwa Chama hicho zilizofanyika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki umekabidhi ofisi kwa chama cha mabalozi Wastaafu nchini (ARTA).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekabidhi ofisi hizo zilizopo katika jengo la Wizara jijini Dar es salaam kwa niaba ya Wizara na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa wizara na watumishi .
Akikabidhi ofisi hizo Balozi Mulamula amesema ofisi hiyo iliyoko katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam itatatumiwa na mabalozi wastaafu hapa nchini ili kuwawezesha mabalozi hao kuendelea kutoa mchango wao katika ujenzi wa Taifa hususani katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.
Akizungumza kwa niaba ya chama cha mabalozi wastaafu Mwenyekiti wa chama hicho Balozi Celestine Liundi amesema chama hicho kwa sasa kina wanachama hai 57 ambao bado wanaweza kuisaidia nchi katika nyanja ya uhusiano wa kimataifa.
Balozi Liundi ameushukuru uongozi wa Wizara kwa kitendo cha kuwapatia ofisi ndani ya jengo la Wizara na kuongeza kuwa kitendo hicho kimewatia moyo wa kuendelea kutoa ushauri,mapendekezo na michango ya mawazo katika kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Mataifa mengine.
WAZIRI MULAMULA AAGANA NA BALOZI WA KENYA NCHINI
Balozi wa Kenya ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Dan Kazungu akizungumza alipofika katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagana na Mhe Waziri. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameagana na Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Dan Kazungu ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini walipokutana katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na balozi Kazungu Waziri Mulamula ameelezea kuridhishwa kwake na utendaji kazi uliotukuka wa Balozi Kazungu ambao umewezesha Tanzania na Kenya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kindugu, kijirani na kijamii ambao umekuwepo siku zote.
Amesema uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Kenya ni jambo lililochochewa na kazi nzuri iliyofanywa balozi Kazungu nchini na kuchochea ukuaji wa biashara, uwekezaji na ustawi wa jamii katika nchi hizo na amemuomba Balozi huyo kuwa balozi mzuri wa Tanzania pindi atakaporejea nyumbani kwao Kenya.
“Katika kipindi chako cha uwakilishi umeiwakilisha vyema Kenya hapa nchini na kuonesha mafanikio makubwa ambayo Tanzania na Kenya tumeyapata kwa pamoja, kazi yako imechochea ukuaji wa biashara uwekezaji na hata ustawi wa jamii katika nchi zetu, nikuombe ukawe balozi mzuri wa Tanzania nchini Kenya’, alisema Mhe. Waziri.
Naye Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Dany Kazungu amesema anajivunia uwepo wake hapa nchini, amejifunza mengi ikiwemo kuthamini utu na ukarimu wa Watanzania, na amewashukuru Watanzania kwa upendo mkubwa waliomuonesha katika kipindi cha miaka minne aliyokuwepo nchini.
"shukurani nyingi kwa upendo wenu Watanzania, mhe. Waziri niwaombee heri na baraka zote katika harakati za kuijenga Tanzania, ni wakati mgumu kusema kwaheri lakini hakuna budi, tuendeee kushirikiana na tufanye kazi pamoja ili kuleta maendeleo ya watu wetu, siku zote nitakumbuka utu na ukarimu wa Watanzania, mnathamini utu hakuna kukwezana, nimejifunza hili toka kwenu," alisema Mhe. balozi Kazungu